Kilichowapata Wema na Amber Rutty kwa kuweka picha na video za ngono mtandaoni

562
0
Share:
Share this
  • 502
    Shares

Msanii wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ameitwa na kuhojiwa na Baraza la Filamu Tanzania kufuatia picha na video zake zenye maudhui ya kingono kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakati akizungumza na kituo cha runinga cha EATV na kueleza kuwa wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliovujisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni, kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo, bila kuangalia nani aliyefanya.

Wakati hayo yaikiendelea kwa Wema Sepetu, msanii mwingine ambaye hivi karibuni video zake za ngono zimesambaa mitandaoni, Amber Rutty amejikuta matatizoni huku Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) likisema kuwa halimtambui mtu huyo kuwa ni msanii kwa sababu hajasajiliwa.

Aidha, Shonza amesema kwamba, wasanii hao wataitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa hatua zaidi, huku akiwataka wasanii kutumia mitandao kuelimisha jamii badala ya kubomoa maadili na tamaduni za kitanzania.

Comments

error: Content is protected !!