Ku-bet kunavyochangia kuathiri afya ya akili kwa vijana

385
0
Share:
Share this
  • 311
    Shares

Vijana wametakiwa kujiepusha na matumizi ya dawa ya kulevya, makosa ya kimtandao, kucheza kamari na kukaa katika magenge yanayoweza kupelekea kupata fikra mbaya zinazoweza kusababisha kuathirika kwa afya ya akili.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Bakari Kambi jijini Dodoma wakati akitoa tamko la kuadhimisha siku ya akili ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Oktoba 10.

“Utumiaji wa mihadarati kuwa ni changamoto kubwa inayowakabili vijana katika mataifa yote pia utumiaji wa dawa za kulevya nayo imehusishwa kwa kiasi kikubwa na tabia hatarishi za ngono zembe na ajali za barabarani” alisema Prof. Kambi.

Prof Kambi amesema kuwa sambamba na elimu kwa umma wizara itaendelea kutoa matibabu ya afya ya akili katika hospitali zote nchini pamoja na kuendelea kutoa dawa za Methadone kwa watumiaji wa dawa za kulevya katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma.

Aidha Prof. Kambi amesema kutokana na tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinazoonesha vijana wanaoathirika na kupata matatizo ya wale walio katika umri wa kuanzia miaka 14, lakini wengi wao hawapati nafasi ya kutambulika na kupata matibabu katika wakati muafala.

“Tafiti za WHO zinaonesha takribani nusu ya magonjwa yote ya akili huanzia katika umri wa miaka 14 ambapo magonjwa ya akili na matumizi ya vilevi ni miongoni mwa changamoto kubwa sana za kiafya na kiusalama zinazoathiri rika hili,” amesema Prof. Kambi.

Prof. Kambi amesema kuwa, kujiua kunaaminika kuwa ni chanzo kikuu cha pili cha vifo vyote vinavyowakabili vijana wengi duniani na Ugonjwa wa Sonona (Depression) umetajwa kushika nafasi ya tatu duniani katika magonjwa yote yanayoathiri vijana duniani.

Kwa mujibu wa Prof. Kambi, takwimu za mwaka 2015 hapa nchini zinaonesha vijana kuanzia miaka  13 hadi 17 walioko shule za misingi na sekondari zinaonesha kuwepo na dalili za Sonona, ambapo vijana zaidi ya asilimia 7 walionesha kuwa na dalili.

Kwa upande wake mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Mirembe, Dkt. Damas Andrew amesema matatizo ya unywaji pombe, uvutaji wa sigara yalitaarifiwa kwa kiwango sawa cha asilimia 5, huku kuvuta bangi kukiwa asilimia 3.1 katika maisha ya wagonjwa.

“Vijana wote waliohojiwa waliripoti kufanyiwa uonevu na wenzao ama kwa kupigwa, kusukumwa au kufungiwa madarasani kunakope kupata athari ya akili”. Amesema Dkt. Damas

Dkt. Damas amesema utafiti umeripoti kuwepo kwa matukio mbalimbali ya ukatili kwa vijana kutoka kwa wazazi na walezi yanayosab kuzorotesha ya akili kwa watoto na vijana wanaowalea.

Vilevile kiwango kikubwa cha unyanyasaji kimeripotiwa kufanyika katika dhidi ya watoto na vijana na kufanya changamoto hizi kuathiri kwa kiasi kikubwa afya ya akili.

Comments

error: Content is protected !!