Kutoweka kwa Mo Dewji, Msemaji wa Simba Haji Manara akamatwa na Polisi

507
0
Share:
Share this
  • 765
    Shares

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara anashikiliwa na Polisi kwa kusambaza taarifa za kutekwa kwa Mfanyabiashara Mohammed Dewji katika mitandao ya kijamii, kwa madai ametumwa na familia jambo ambalo sio kweli.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kushikiliwa kwa Manara ambapo ameeleza kuwa, uchunguzi dhidi yake utafanyika.

“Manara tunamshikilia kwa uchunguzi zaidi yeye amekuwa akisambaza taarifa mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ametumwa na familia, lakini sio kweli, hajatumwa na familia hivyo tunamshikilia,” amesema Kamanda Mambosasa.

Akizungumza na wanasimba jana kuhusu tukio la kutekwa kwa Mo Dewji, Manara alisema kwamba tukio hilo limemshtua kila mmoja, na kwamba wanaliachia jeshi la pozi kazi ya kumtafuta wakiamini kwamba atapatikana akiwa hai.

“Wanasimba wawe watulivu wakiliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kwamba wanaamini MO atapatikana akiwa hai,” alisema Manara.

Hadi sasa saa 40 zimeshapita tangu mfanyabishara huyo alipotekwa jana katika Hoteli ya Colosseum alipokuwa anakwenda kufanya mazoezi.

Comments

error: Content is protected !!