Maagizo ya RC Makonda kwa watendaji wa mabasi ya mwendokasi kuhusu utoaji huduma

358
0
Share:
Share this
  • 571
    Shares

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameonyesha masikitiko yake kwa namna mradi wa mabasi yaendayo haraka Mwendokasi namna unavyoendeshwa na kuwataka watendaji wote kukutana naye Kimara Kesho asubuhi saa 12.30.

“Sifurahishwi na namna mradi wa mwendokasi unavyoendeshwa kwani matarajio ya Mh Rais ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri wa jiji la Dar es salaam ikigeuzwa historia kupitia mradi huu.

Kwasababu hiyo ameagiza watendaji wote wanaosimamia mwendokasi wakutane naye Kituo cha Mabasi Kimara (Kimara Bus Terminal) kesho saa 12.30 asubuhi wamweleze kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukua huku wakishuhudia kero wanazopitia wananchi.

“Nitumie pia fursa hii kuwaomba radhi wananchi kwa kero hii na ninawaahidi kuwa jambo hili litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni. Tukunate Kimara kesho asubuhi”.

Kauli ya RC Makonda imekuwa ikiwa ni siku moja tangu wakazi wa jiji la Dar es Salaam kueleza kero wanazokumbana nazo katika usafiri huo, huku baadhi wakitaka serekali kuwezesha uwepo wa ushindani katika mradi huo, ili kuboresha huduma ya usafiri.


Comments

error: Content is protected !!