Maisha ya Mwalimu Nyerere akifundisha Shule ya Sekondari Pugu

959
0
Share:
Share this
  • 2.8K
    Shares

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyrerere ni mmoja wa viongozi ambao kwa namna mbalimbali walilipigania bara la Afrika wakati wa ukoloni na hata baada ya hapo kuhakikisha kuwa linakuwa huru na kupata maendeleo.

Nyerere ambaye ni Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadae Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitaka Afrika iungane ili kuweza kuwa na nguvu zaidi, lakini tofauti na Nkrumah ambaye alitaka Afrika iungane kwa wakati mmoja, Nyerere alitaka mchakato huo uende taratibu kwa kuanza kwanza na jumuiya za kikanda, kama ilivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Turudi kwenye hoja yetu. Kikubwa ambacho watu wengi hawakifahamu ni kuwa, Hayati Kambarage Nyerere amewahi kuwa mwalimu kabla ya kujikita zaidi katika siasa.

Ni kweli, Nyerere alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Francis Pugu, jijini Dar es Salaam ambapo alifundisha kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya kujiuzulu na kujikita katika siasa.

Wakati akiwa shule hapo, Nyerere alikuwa ndiye mwalimu pekee mzawa, na alikuwa akifundisha masomo ya Baiolojia na Kiingereza. Hii ndio sababu amekuwa akiitwa Mwalimu.

Nyerere aliandika barua ya kujiuzulu 22 Machi 1955 na kueleza sababu kubwa, ni ili aweze kupata muda wa kutosha katika harakati za kisasa ambazo amekuwa akizifanya.

Katika barua yake hiyo, Nyerere aliueleza uongozi wa shule kwamba, amelifikiria chaguo alilopewa, kati ya kazi yake shuleni hapo na uanachama wangu katika TANU na kusema kwamba, amefikia uamuzi kwamba lazima ajiuzulu katika nafasi yake ya kufundisha.

Nyerere alitakiwa kuchagua jambo mboja, kutokana na shughuli zake za TANU kuingiliana na utendaji wake shuleni.

Licha ya kuondoka shuleni hapo, Nyerere aliuomba uongozi wa shule hiyo kuendelea kumuombea na kushirikiana naye katika shughuli hiyo mpya ya kisiasa aliyokuwa akiiendea.

“Nakushukuru wewe na Mapadri wengine kutokana na kushirikiana nami siku zote. Nitazihitaji sala zenu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Endelea, Padri, kuniombea,” aliandika Nyerere.

Comments

error: Content is protected !!