Mambo 7 ambayo Rais Dkt Magufuli amemuagiza Waziri mpya wa Mambo ya Ndani kuyafanya

1338
0
Share:
Share this
  • 682
    Shares
CMTL Group

Jana Julai 1 2018 Rais Dkt John Magufuli alifanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, mabadiliko ambayo yalitangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi. Katika mabadiliko hayo, moja ya walioteuliwa katika nafasi mpya ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Alphaxard Lugola, Mbunge wa Mwibara ambaye anachukua nafasi ya Dkt Mwigulu Nchemba aliyeondolewa katika Baraza la Mawaziri.

Leo Julai 2 2018 Rais amewaapisha viongozi hao wapya na katika hotuba yake fupi baada ya uteuzi ameeleza matarajio yake katika utendaji wao lakini pia masikitiko yake kuhusu utendaji wa waliowatangulia. Moja ya sehemu ambazo Rais Magufuli ameeleza masikitito na matarajio yake kwa kirefu ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Hapa chini ni mambo saba ambayo ameelekeza Waziri mpya Kangi Lugola kuyashughulikia.

 

  1. Kushughulikia maelekezo ya kamati ya Bunge iliyotaka hatua zichukuliwe dhidi ya mkataba wa ufungaji vifaa katika vituo 108 vya Polisi uliogharimu Shilingi Bilioni 37

  2. Kushughulikia uagizaji wa magari 777 ya polisi ambayo yamekwama bandarini na baadhi yake kuonekana yametumika

  3. Kashfa ya ununuzi wa sare za Polisi

  4. Uhaba wa magari katika Jeshi la Zimamoto

  5. Kudhibiti mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo hayana maslahi kwa Taifa

  6. Utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni

  7. Ongezeko kubwa la ajali za barabarani, ambapo amemtaka kuwawajibisha mara moja Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa huo kufuatia ajali 3 zilizotokea mkoani humo na kusababisha watu 40 kupoteza maisha ndani ya wiki mbili.

Comments

error: Content is protected !!