Mawaziri wapelekwa kusuluhisha mgogoro kati ya RC Kilimanjaro na Wakuu wa Wilaya

389
0
Share:
Share this
  • 1.1K
    Shares

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewatuma mawaziri wawili kutoka ofisi ya Rais kwenda mkoani Kilimanjaro ili kutatua tatizo la uhusiano kati ya  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na wakuu wa wilaya ambapo alidokeza kuwa chanzo cha pande hizo kutokuelewana na matumizi ya adhabu ya kuwaweka watu ndani waliyonayo wakuu wa wilaya na mkuu wa mkoa.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo jana Disemba 3, 2018 wakati akifungua mafunzo ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ya Tanzania Bara yaliyolenga kujengeana uwezo jijini Dodoma.

Mawaziri walioagizwa kwenda mkoani Kilimanjaro ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora),  George Mkuchika.

Akitoa maagizo hayo,Waziri Mkuu alitahadharisha kuwa, wakati mwingine kauli na hatua ambazo si muhimu zinaweza kuifanya Serikali kuonekana  si sekta muhimu.

“Mheshimiwa waziri ameeleza hapa juu ya matumizi ya adhabu ya kuweka watu ndani. Tumeona mabishano haya kati ya kiongozi wa mkoa na wakuu wa wilaya wanapochukua hatua lakini bado kuna shida,” amesema Majaliwa.
“Nataka niagize waziri wa TAMISEMI nenda mkoani Kilimanjaro bado kuna shida. Kuna shida ya mahusiano kati ya mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya tena wengi sio mmoja.”
Waziri Mkuu amemuagiza pia Waziri George Mkuchika atakapopata muda kwenda Kilimanjaro, aendeshe semina ya wakuu wa wilaya juu ya itifaki na kuheshimu mamlaka ya watu wengine, ili kuwezesha mkoa kufanya kazi yake vizuri.

Comments

error: Content is protected !!