Mawaziri watano wanaoongoza kwa utoro bungeni

518
0
Share:
Share this
  • 509
    Shares

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (Mb) leo ameweka wazi mahudhurio ya wabunge katika vikao vya kamati za Bunge na mahudhurio kwenye vikao vya na Bunge, ambapo amewataja mawaziri watano ambao mahudhurio yao hayaridhishi kama wengine.

Akizungumza baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Alhamisi Novemba 15, 2018, Ndugai amewataja mawaziri hao wenye uhudhuriaji mdogo kuwa ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (45) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (41).

Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi (38), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba (37) na Waziri wa Mambo ya Mambo nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga aliyepata asilimia tano.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametajwa kuwa ndiye waziri mwenye mahudhurio makubwa zaidi.

Spika amesema mahudhurio hayo ni ya vikao vya kamati za Bunge 33 vya Machi, Agosti na Oktoba na vikao 61 vya mkutano wa 11 wa Bunge ambao ulikuwa wa bajeti na vikao tisa vya Bunge la 12.

Spika amesema japo wakati mwingine mawaziri hushindwa kuhudhuria kutokana na shughuli nyingine zinazowakabili, lakini ni vyema wakatoa taarifa.

Kwa upande wa wabunge, Godbless Lema (Arusha Mjini- Chadema) ndiye anayeongoza kwa mahudhurio hafifu kwa vikao vya kamati na Bunge amehudhuria kwa asilimia 7.8 tu.

Wabunge wengine walio katika mahudhurio ya chini kabisa ni Salim Hamis Salim (Meatu-CCM); Mansour Yusuph Himid (Kwimba-CCM); Abdul Azizi (Morogoro-CCM); Hussein Nassoro Amar (Nyangwale-CCM); Mbaraka Bawazir (Kilosa-CCM); Dk Mathayo David (Same Magharibi-CCM).

Wengine John Mnyika (Kibamba- Chadema); Salim Hassan Turky (Mpendae-CCM) na Suleiman Nchambi (Kishapu-CCM).

Comments

error: Content is protected !!