wekeza

Mbunge Zitto Kabwe ajificha ndani ya Bunge hadi sasa, ahofia kukamatwa akitoka

517
0
Share:
Share this
wekeza

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amejificha ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma hadi sasa kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mara tu atakapotoka nje ya ukumbi huo.

Mbunge huyo machachari amejikuta jatika hali hiyo baada ya kile alichoeleza kuwa alihoji kuhusu hatua za ukamatwa wa mbunge katika viunga vya bunge kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Mbunge Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa alianzisha majadali bungeni kuhusu hatua za kukamatwa kwa wabunge wakati bunge likiendelea. Alisema kuwa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth) Spika wa Bunge anatakiwa kutoa idhini ya kukamatwa kwa mbunge.

Hoja ya Zitto Kabwe imekuja siku moja baada ya Mbunge Tundu Lissu kukamatwa mara tu alipotoka nje ya ukumbi wa bunge jana jioni na kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam usiku. Zitto alisema kuwa mwaka jana, Mbunge Godbless Lema ambaye bado yupo rumande naye alikamatwa vivyo hivyo.

Aidha, ameandika kuwa Polisi wa bunge wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye hafahamu ni lipi.

Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku katika kituo cha runinga cha Azam Two, Mbunge huyo bado yupo ndani ya ukumbi wa bunge akihofia kuwa polisi watamkamata mara tu atakapotoka ndani ya ukumbi huo kama ilivyokuwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu.

Kwa upande mwingine wabunge wa upinzani walitoka nje ya ukumbi wa bunge wakati wa kikao cha leo jioni kufuatia amri ya Naibu Spika Dkt Tulia Ackson kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni vurugu zilizoanzishwa na Mbunge wa Kawe, Halima James Mdee.

Comments

error: Content is protected !!