Mchungaji awalisha waumini wake mende

601
0
Share:
Share this
  • 676
    Shares

Mchungaji mmoja nchini Afrika Kusini amewalisha waumini wake wawili mende, huku wenyewe wakidai kuwa, mende huyo alikuwa na ladha ya jibini na mwingine akidai alinukia kama viungo vya chakula.

Tukio la kuwalisha waumini wake wadudu hao limetokea takribani miezi minne tangu Mchungaji huyo, Penuel Mnguni tangu alipotangaza kuwa, kuwalisha watu nyoka ni kinyume na biblia.

Kanisa lake linalofahamika kwa jina la End Times Disciples Ministries liliweka taarifa hiyo katika ukurasa wa facebook na kusema kuwa, mchungaji huyo aliwaita mende wakatokea kanisani.

Baada ya mende huyo kutokea kanisani, aliwaita waumini wawili ambao waligawana na kuanza kumla mende huyo huku muumini mmoja aliyefahamika kwa jina la Charles alisema ilikuwa na ladha mithili ya jibini isiyo ya kawaidana kwa upande wa Eric ilikuwa kama kiungo cha chakula.

Katika taarifa hiyo, kanisa hilo limeeleza kwamba, baada ya waumini hao kula mdudu huyo, kiwango chao cha kufundisha hakitakuwa tena cha kawaida.

Katika taarifa nyingine, kanisa hilo limesema kuwa mchungaji huyo aliombea ua lenye sumu na muumini mmoja akalila kiasi kwamba alifurahia na kuomba ale lote peke yake.

Mchungaji huyo amewahi kuzua gumzo nchini Afrika Kusini ikituhumiwa kuwalisha waumini wake nyoka, panya na nywele.

Mashtaka yaliyokuwa yamefunguliwa dhidi yake yalitupiliwa mbali mwaka 2015 baada ya kukosekana ushahidi.

 

Comments

error: Content is protected !!