Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Acacia akamatwa na Polisi

463
0
Share:
Share this
  • 334
    Shares

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imesema kuwa kwa siku za hivi karibuni watendaji wake hasa wa Mgodi wa North Mara na waliopo katika ofisi ya Dar es Salaam wamekuwa wakishinikizwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na mamlaka nyingine za serikali kutoa taarifa.

Katika taarifa yake ya Oktoba 10 mwaka huu kampuni hiyo imeseema kwamba, taarifa ambazo watendaji hao wanatakiwa kutoa ni za matukio ya nyuma wakati kamouni hiyo ilipokuwa ikifahamika kama African Barrick Gold. Aidha wameeleza kuwa, taarifa nyingi ambazo zinahitajika sasa wamewahi kuzitoa.

Watendaji hao wa Acacia wamekuwa wakihojiwa na kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda mrefu, na katika baadhi ya nyakati wameshindwa kutoa taarifa walizotakiwa, kutokana na tarifa hizo ama kutokuwepo au kutoruidhisha mamlaka za serikali, na hivyo kufikia hatua ya watendaji hao kutishiwa.

Wiki iliyopita TAKUKURU walifika katika ofisi za Dar es Salaam za kampuni hiyo na kuchukua kompyuta 3 jambo ambalo kampuni hiyo imesema haikuona haja yakufanya hivyo na kwamba wanaendelea kufuatilia tukio hilo.

Usiku wa Oktoba 9, Meneja Biashara wa Acacia, Maarten van der Walt alilala rumande baada ya kukamatwa na Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime akihusishwa na makosa yaliyofanya na kampuni hiyo mwaka 2013. Hadi jana meneja huyo alikuwa bado yupo rumande licha ya kupewa dhamana kutokana na kutakiwa kuhakiki pasi yake ya kusafiria.

Aidha, kampuni hiyo imesema inaendelea kufuatilia kwa makini tuhuma hizo zilizoibuliwa na mamlaka za serikali. Pia imeeleza kuwa  hatua zinazochukuliwa kama kumshikilia kiongozi wa kampuni ni jambo ambalo limekuwa na athari za kiutendaji kazi.

 

 

Comments

error: Content is protected !!