Mfanyabiashara Yusuf Manji kufilisiwa mali zake

471
0
Share:
Share this
  • 1.1K
    Shares

Dar es Salaam: Mali za mfanyabiashara maarufu Afrika, Yusuf Manji zipo hatarini kupigwa mnada ya Benki ya Biashara ya Maendeleo Afrika Mashariki na Kusini, endapo bilionea huyo atashindwa kulipa madeni anayodaiwa na benki hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Disemba 5, 2018  na wafisili na wakabidhi wasii waliopo chini ya Kampuni ya Price Water House Coopers (PWC), imeeleza kuwa, kuanzia jana, mfanyabiashara huyo hataruhusiwa kumiliki mali hizo hadi atakapolipa madeni hayo, na sasa zimewekwa chini ya  David Tarimo na Nelson Msuya.

Mameneja hao wawili wameteuliwa na benki hiyo kuweza kukusanya madeni yote kutoka kwa Manji, na endapo atashindwa kulipa, mali zake ikiwemo jengo la la Quality Center lililopo Barabara ya Nyerere (zamani Barabara ya Pugu) jijini Dar es Salaam linalomilikiwa na Quality Group Ltd.

Wafilisi na wakabidhi wasii hao zimesema wanayo dhamana ya kumiliki hati za mali zinazohamishika na zisizohamishika ili kurejesha madeni anayodaiwa mfanyabiashara huyo na benki iliyotajwa hapo juu kama mdeni atashindwa kulipa.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, walipouliza kiasi cha madeni anayodaiwa Manji na benki hiyo, Tarimo wa PWC alisema hawezi kutaja kwa kuwa itakuwa ni kwenda kinyume na maadili ya kazi yao.

 

Comments

error: Content is protected !!