Mkaguzi Mkuu: Taasisi hizi zinalipa mishahara chini ya kiwango

365
0
Share:
Share this
  • 325
    Shares
CMTL Group

Kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, Bunge na maeneo mbalimbali, jambo kubwa linalojadiliwa sana kwa sasa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa hivi karibu.

Ripoti hiyo imesheni mambo mbalimbali kufuatia ukaguzi uliofanywa katika taasisi mbalimbali ndani ya serikali kuu na serikali za mitaa, balozi, mashirika na vyama vya siasa hadi kufiki Juni mwaka 2017.

Katika ukaguzi wa mishahara ya watumishi wa umma, CAG, Prof. Juma amebaini kuwa, baadhi ya Taasisi zina watumishi wanaopokea mishahara chini ya kiwango kinachokubalika, kinyume na kifungu namba 3 cha Sheria ya kurejesha Madeni ya mwaka 1970 na Waraka wa Serikali wenye kumbukumbu namba C/CE.45/271/01/1/87 wa tarehe 19 mwezi wa tatu 2009.

CAG amesema kuwa, waraka huo ulitolewa na  Katibu mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora ukiwaelekeza Maafisa Masuuli wote kuhakikisha kuwa, makato yote ya mishahara ya watumishi kwaajili ya marejesho ya madeni katika mwezi yasizidi moja ya tatu ya mshahara wa mtumishi kwa mwezi.

Katika ukaguzi wa wa taasisi 12, amebaini kuwa nimegundua kuwa, watumishi 278 wanapokea mishahara chini ya kiwango  kinachokubalika kisheria.

Aidha, amesema hali hiyo inasababisha watumishi kukosa ari ya kufanya kazi, hivyo kushusha ufanisi. Hii huwafanya watumishi kutokuwa na uhakika na kipato chao kazini.

Kutokana na ripoti zilizopita, CAG amesema kuwa, idadi ya watumishi wanaopokea mshahara chini ya kiwango kinachokubalika kisheria imeongezeka kutoka watumishi 49 hadi kufikia 278, na idadi ya taasisi pia zimeongezeka kutoka sita mpaka kufikia kumi na mbili mwaka huu.

Katika kutoa ushauri kuhusu namna ya kukabiliana na hali hiyo, CAG amewataka Maafisa Masuuli kuimarisha udhibiti wa ndani kwa kuthibitisha mikopo yote ya watumishi kabla ya kutoa mkopo mwingine na kuwasiliana na watoaji wa mikopo ili makato yasizidi moja ya tatu ya mshahara wa mtumishi kwa mwezi.

“Ninashauri Taasisi zote kufuata Kanuni na miongozo ya Serikali kwa kuchunguza na kuhakikisha mishahara na makato ya watumishi kabla ya kutoa mkopo kwa watumishi,” amesema CAG.

Comments

error: Content is protected !!