Mlima Kilimanjaro washinda tuzo kubwa Afrika

847
0
Share:
Share this
  • 1.4K
    Shares
CMTL Group

Mlima Kilimanjaro umeshinda tuzo kubwa barani Afrika kwa kuwa, Kivutio Bora cha Utalii Afrika kwa mwaka 2017, tuzo ambayo hutolewa kila mwaka na World Travel.

Mlima Kilimanjaro ambano ndio mlima mrefu zaidi barani Afrika, umevishinda vivutio vingine ambavyo ni Ngorongoro Crater iliyopo Tanzania, Pyramids of Giza nchini Misri, Kisiwa cha Robben, Table Mountain na V&A Waterfront vyote vya Afrika Kusini.

Tuzo hii ni ya tatu mfululizo kwa Mlima Kilimanjaro kwani ilishinda mwaka 2015, 2016. Mbali na miaka hiyo, mlima huo ulitwaa tuzo hiyo mwaka 2013, lakini mwaka 2014, Table Mountain, ya Afrika Kusini iliibuka mshindi.

Mbali na hilo, vivutio mbalimbali vya Tanzania vimetajwa katika vipengele mbambali kuwani tuzo za masuala mbalimbali ya utalii duniani.

Mlima Kilimanjaro umetajwa kuwania pia tuzo ya Kivutio Bora cha Utalii Duniani kwa mwana 2017.

Comments

error: Content is protected !!