Mmiliki wa Leicester City afariki katika ajali ya helikopta

284
0
Share:
Share this
  • 335
    Shares

Mmiliki wa Klabu ya Leicester amethibitishwa kufariki dunia baada ya helikopta aliyokuwa amepanda kuanguka na kuwaka moto muda nje ya uwanja wa klabu hiyo mfupi baada ya kupaa Oktoba 27.

Bilionea huyo kutoka nchini Thailand, Vichai Srivaddhanaprabha amefariki dunia pamoja na watu wengine wanne ambao wawili ni marubani wa helikopta hiyo na wawili ni wafanyakazi wake.

Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa, muda mfupi baada ya helikopta hiyo kutoka ndani ya uwanjwa wa klabu hiyo, King Park, ilianza kuyumba na kuanguka nje kidogo na kisha kuwaka moto.

Jeshi la Polisi katika mji huo limesema linaamini kuwa waliofariki pamoja na bilionia huyo ni wafanyakazi wake wawili, Nursara Suknamai na Kaveporn Punpare pamoja na marubani wawili, Eric Swaffer na Izabela Roza Lechowicz ambao walikuwa ni wapenzi.

(L-R) Izabela Roza Lechowicz, Eric Swaffer, Nursara Suknamai and Kaveporn PunpareKutoka kushoto ni Izabela Roza Lechowicz, Eric Swaffer, Nursara Suknamai na Kaveporn Punpare

Bilionea huyo hiyo alikuwa ametoka kuangalia mchezo wa ligi kuuu ya Uingereza kati ya klabu yake na West Ham United ambao ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya 1-1

Vichai Srivaddhanaprabha mwenye miaka 60 akiwa na mke na watoto wanne aliinunua klabu hiyo kwama 2010 kwa shilingi bilioni 115 (£39m).

Chini ya uongozi wake, kalbu hiyo ilifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2016. Katika taarifa yake, klabu hiyo imesema kuwa sala na mawazo yao yapo pamoja na familia kufuatia vifo hivyo.

Hundreds of bouquets of flowers and tributes have been left by Leicester City fansWananchi wakiweka maua nje ya uwanja wa Leicester City baada ya ajali hiyo

Leicester City King Power Stadium helicopter crashMabaki ya helikopta hiyo baada ya kuanguka na kuwaka moto

Klabu ya Leicester City ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa EPL, ikiwa na alama 13 baada ya kushuka dimbani mara 10.

 

Comments

error: Content is protected !!