Mtanzania akamatwa Kenya akiwa ameficha dawa za kulevya kwenye njia ya haja kubwa

369
0
Share:
Share this
  • 425
    Shares

Nairobi: Mamlaka nchini Kenya zinawasikia watu watatu akiwemo raia mmoja wa Tanzania, baada ya kukutwa na dawa za kulevya wwalizokuwa wakizisafirisha kwenda China na Ugiriki.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) amesema kuwa maafisa wake waliwashuku watu hao walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi alhamisi usiku wakati wakijiandaa kwenda China na India.

Mtanzania huyo aliyefahamika kwa jina la Msafiri Musa alikuwa ameficha tembe 69 za dawa za kulevya ambazo hazijatambulika katika njia yake ya haja kubwa ili kuepuka kubainika, alisema DCI.

Uwanja wa huo wa ndege, ambao ndio unaohudumia watu wengi zaidi Afrika Mashariki kwa miaka ya hivi karibuni ulikuwa uchochoro wa kusafirisha dawa za kulevya kwenda katika nchi mbalimbali Ulaya na masoko mengine duniani, licha ya kuwa polisi waliongeza ulinzi.

Ukamataji huo umekuja ikiwa ni wiki mbili tu tangu polisi katika uwanja huo walipokamata dawa nyingine za kulevya aina ya heroin na methamphetamine zilizokuwa zikisafirishwa kwenda China na Ugiriki.

Comments

error: Content is protected !!