Mtanzania ateuliwa kuongoza shirika la Umoja wa Mataifa (UN)

461
0
Share:
Share this
  • 828
    Shares

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

Bi Msuya amekuwa Naibu Katibu Mkuu na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ambalo lina makao makuu yake jijini Nairobi, Kenya.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amenukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa akisema, Antonio Guterres amechukua hatua hiyo huku akiendelea kumtafuta mkuu wa kudumu wa UNEP.

Bi. Msuya ameteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, Erik Solheim kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha, ambapo imeripotiwa kwamba alitumia TZS bilioni 1.2 katika safari kwa kipindi cha miezi 22.

Mbali na safari hizo, kiongozi huyo hawakupo ofisini kwake mara nyingi ambapo ni sawa na asilimia 80 ya muda wake wa kazi.

Hadi wakati wa kuteuliwa kwake, Bi Msuya alikuwa mshauri wa Makamu Rais wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa Asia Mashariki na Pacific jijini Washington DC wadhifa alioushikilia tangu mwaka jana.

Bi. Msuya ana shahada ya uzamivu kwenye masuala ya sayansi ya biolojia ya viumbe viini na viumbe vidogo pamoja na sayansi ya kinga mwilini kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada.

Ana shahada ya kwanza katika Biokemia na Kinga Mwilini kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, Scotland.

Bi Msuya ameolewa na ana watoto watatu.

Comments

error: Content is protected !!