Mtendaji Mkuu wa mabasi ya mwendokasi atakiwa kujieleza

274
0
Share:
Share this
  • 288
    Shares
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi (DART), Ronald Lwakatare kujieleza mara moja ni kwanini huduma za usafiri zinasuasua na kusababisha adha kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia amemtaka Naibu Waziri TAMISEMI, Joseph Kakunda kukutana na Menejiment ya DART pamoja na UDART kesho ili kujua nini kiini cha matatizo yanayoukumba usafiri huo na kupelekea huduma mbovu.

Aidha, Waziri Jafo amemtaka Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Musa Iyombe kuchunguza kama kuna watendaji wa DART wanaohujumu mradi huo na wachukuliwe hatua za haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.

Comments

error: Content is protected !!