Nafasi mbalimbali za ajira kutoka Wizara ya Utumishi wa Umma

Share:
Share this
CMTL Group

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Taasisi za Umma mbalimbali Serikalini, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 31 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.1 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – MAABARA YA MAJI (LABORATORY TECHNICIAN WATER II) – NAFASI 9

1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kufanya mchanganuo (analysis) kikemikali ili kuthibitisha/kutathmini vielelezo (samples) vinavyohusika kwenye maabara;
 2. Kutunza vyombo vya maabara;

iii. Kutayarisha vitendea kazi vya maabala kwenye masomo ya sayansi kwa vitendo

 1. Kutambua, Kuthibitisha na kuweka kumbukumbu za takwimu za vielelezo mbalimbali;
 2. Kusaidia kazi za watafiti.

1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (vi) waliofuzu mojawapo ya mafunzo ya miaka miwili (2) ya Stashahada (Diploma) ya ufundi sanifu wa Maabara ya maji au sifa zinazolingana na hizo kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara wa Serikali yaani TGS C

1.2 FUNDI SANIFU (HAIDROLOJIA) DARAJA LA II (TECHNICIAN GRADE II HYDROLOGY) – NAFASI 15

1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji;
 2. Kutunza takwimu za maji;

iii. Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro;

 1. Kuchora ‘hydrograph’ za maji;
 2. Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k;
 3. Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa;

vii. Kuingiza takwimu kwenye kompyuta;

viii. Kufundisha wasoma vipimo.

1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi (FTC- Hydrology) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.2.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

1.3 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – HAIDROJIOLOJIA (TECHNICIAN GRADE II – HYDROGEOLOGIST) – NAFASI 7

1.3.1 MAJUKUMU YA KAZI

 1. Kuhakiki uwezo wa kisima kutoa maji (Pump test);
 2. Kuchora ramani za awali za kiufundi;

iii. Kuhifadhi taarifa za kikazi (Field Data) zipatikanazo wakati wa utafiti wa maji chini ya ardhi.

1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi (FTC HYDROGEOLOGY) au Stashahada ya Kawaida ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.3.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

 1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
 2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

 1. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
 2. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita vilivyothibitishwa (Certified Copies) kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

– Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

– Computer Certificate

– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

– Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.

 1. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

 1. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
 2. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
 3. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Mei, 2018.

xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa

Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU VILIVYOTHIBISHWA (CERTFIED). BARUA HIYO IELEKEZWE KWA

KATIBU,

OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

S.L.P 63100

DAR ES SALAAM.

KATIBU

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Comments

error: Content is protected !!