Namna ya kuepuka utapeli unaofanyika kupitia simu za mkononi

2075
0
Share:
Share this
  • 3K
    Shares

Epuka matapeli kupitia simu za mkononi

Utapeli unavyokuja

1. Unapokea SMS kutoka namba ya simu usiyoifahamu. SMS kama “Ile pesa tuma namba hii (wanakuwekea namba) line yangu ina matatizo upande wa kupokea pesa.” au “Umeshinda bahati nasibu, tuma asilimia fulani ya pesa ili upate zawadi yako”, au “Ile dawa mpya imewasili mjukuu wangu njoo uchukue”, na jumbe nyingine kama hizo

2. Wewe bila kufikiria mara mbili kwamba nani ulikuwa na miadi naye kumtumia pesa au kupiga namba husika kuhakiki, unatuma pesa

3. Tapeli yule anaipokea pesa na kuitoa kisha line huenda hataitumia tena. Inakubidi kutoa taarifa kwenye mtandao husika kwamba umetapeliwa suala ambalo linachukua muda ikiwemo kutoa taarifa polisi na upelelezi kufanyika utaratibu wa kisheria ambao kama unavyofahamu unahitaji umakini na huchukua muda. Muda mwingi unapotea na unapata usumbufu

Namna ya kuepuka kero hii

1. Usitoe namba yako ya simu sehemu ambazo huzifahamu au zisizo za lazima. Mawasiliano yako ni binafsi isipokuwa kama unafanya biashara au shughuli ambayo inakuhitaji kutoa namba yako ya simu maeneo mbalimbali. Sehemu hatari kuweka namba zako hovyo ni kujiunga na makundi mitandaoni ambao hufahamu watumiaji wake, mfano makundi ya WhatsApp, kundi moja la WhatsApp lina watu 256, kama unamfahamu mtu mmoja tu maana yake kuna watu 254 usiowafahamu wanapoishi wala shughuli zao ambao tayari umewapa namba yako ya simu bila kujua. Maeneo mengine ni kama Facebook, Instagram, Twitter, madaftari ya wageni kwenye ofisi mbalimbali, nyumba za wageni, na kadhalika. Kama namba yako si lazima, usiitoe.

2. Kabla ya kutuma pesa sehemu yoyote jiridhishe kwamba unayemtumia pesa unamfahamu au una biashara au sababu maalumu ya kumtumia fedha.

3. Ikitokea unayetaka kumtumia fedha amebadilisha namba ya kupokelea fedha, usikubali maelezo ya SMS pekee kwamba tuma huku bali mpigie na jiridhishe kwamba ndiye na namba mpya aliyotuma ni sahihi.

4. Toa taarifa kwa mtandao wako kama namba inakusumbua mara kwa mara kukutumia SMS za “Ile pesa tuma namba hii au ile”.

*SHARE* ujumbe huu na wengine

Comments

error: Content is protected !!