Nandy na Aslay matatani kwa tuhuma za kuiba wimbo

1071
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri kwa hivi sasa Aslay pamoja na msanii wa kike mwenye sauti ya kipekee kutoka THT, Nandy wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kutishiwa kuburuzwa mahakamani baada ya kukopi wimbo bila ruhusa.

Aslay na Nandy kwa sasa wanatamba na kibao chao kinachoitwa ‘Subalkheri Mpenzi’, kibao ambacho kinafanya vizuri katika chati mbali mbali za stesheni za redio, runinga na hata kukaa katika nafasi za mwanzoni katika mtandao wa YouTube.

Kwenye ziara na vyombo vya habari ‘media tour’ waliyofanya katika jitihada za kutangaza nyimbo hiyo, Aslay na Nandy waliwahakikishia mashabiki zao kuwa wamepata ruhusa kamili ya kurudia na kuuimba wimbo huo ambao ulishawahi kuimbwa siku za nyuma.

Sintofahamu imekuja kuibuka baada ya mmiliki wa wimbo hu, kikundi cha Taarab asilia Visiwani Zanzibar (Culture Music club), kudai kuwa hawazitambui pesa zilizotolewa jumla ya shilingi 800,000 kama fidia ya wimbo wao kutumiwa na hivyo wanajipanga kuwafikisha mbele ya mahakama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Katibu Mtendaji wa kikundi hicho, Taimur Rakuni amedai kuwa wasanii hao kabla ya kuimba wimbo huo upya walitakiwa kuonana na uongozi huo, ili kukubaliana jambo ambalo hawakulitekeleza.

Kwa msanii Aslay hii ni mara ya kwanza kwake kukumbana na skendo ya namna hii ya kutumia wimbo wa wasanii wengine bila idhini ya mmiliki, lakini kwa Nandy ametuhumiwa mara nyingi na wasanii wengine kwa kuiba nyimbo na kuzirudia bila ruhusa, mfano Ray C ambaye alimjia juu na kudai kaiba wimbo wake na kuuimba bila ruhusa.

Comments

error: Content is protected !!