Njia ya kuweka Instagram Stories zako zionekane na watu unaowataka tu

210
0
Share:
Share this
  • 125
    Shares

Instagram ni miongoni mwa mitandao mingi kama vile Twitter na Facebook ambayo kwa muda watu wamekuwa wakifahamu kwamba, kila wanachokiweka humoo, kinaonekana na watu wengi. Lakini ukweli ni kwamba, kuna mifumo iliyowekwa katika mitandao hii ya kuwawezesha wale tu ukaoamua waone unachoweka.

Kwa upande wa Instagram Stories, watu wengi hufurahi wanapopata wafuasi wengi kutazama picha zao. Lakini kuna wakati mtu huweka picha zake ambazo asingependa kila mtu aone, bali watu wachache wa karibu tu.

Hilo si tatizo tena kwani juma hili Instagram imezindua huduma hiyo ili ukiweka picha au video zako ambazo ni personal uchague watu ambao wataziona, lakini wakati huo huo bila kufanya akaunti yako kuwa private.

Huduma hiyo ambayo inaitwa ‘Close Friends’ inakupa wewe uwezo wa kuchagua kama unachokiweka katika Instagram Story yako kionekane na watu wote, au wachache unaowataka. Hakuna mtu atajua amechaguliwa, na wale ambao hutawachagua, hawatajua kama umeweka kitu chochote.

Jinsi ya kutengeneza orodha hiyo, bonyeza sehemu yenye picha yako katika akaunti yako ya Instagram, itafunguka sehemu ya kupiga picha au kurekodi video, lakini upande wa juu kushoto mwa simu yako kuna ‘icon’ ya ‘setting’, ibonyeze.

Baada ya hapo utaona sehemu imeandikwa ‘close friend’, ukibonyeza hapo itakuletea majina ya watu wako ambapo unaweza kuchagua wataaoona utakachoweka kwenye Instagram Story yako. Kumuweka mtu kwenye orodha yako bonyeza kitufe ‘add’ pembeni ya jina la mtu, au bonyeza kwenye mapendekezo (suggestions) ambapo Instagram itakuletea majina ya watu ambao unawasiliana nao mara mara.

Baada ya hapo wakati ukirekodi story, itaona sehemu imeandikwa Close Friend, ukiibonyeza, ulichorekodi au kuweka kitakwenda kwa uliowachagua tu.

Comments

error: Content is protected !!