Nyoka atafuna mamilioni na kutoweka

407
0
Share:
Share this
CMTL Group

Karani wa mauzo nchini Nigeria amefukuzwa kazi baada ya kuwaambia wakaguzi wa hesabu kuwa fedha kiasi cha Naira milioni 36 (sawa na shilingi za Tanzania milioni 226.2) zimemezwa na nyoka.

Karani Philomena Chieshe anayefanya kazi katika Ofisi ya Bodi ya Mitihani nchini Nigeria, alimtupia lawama nyoka huyo kuwa amekula kasi hicho cha fedha ambazo zilikuwa zimekusanya kutokana na ada ya kujiandikisha iliyolipwa na wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo vikuu nchini humo.

Bodi hiyo imeeleza kuwa wamepuuzia sababu zilizotolewa na karani huyo na tayari wameanza kumchukulia hatua za kisheria juu ya upotevu wa fedha hizo.

 

Comments

error: Content is protected !!