Picha: Diamond hadharani kwa mara ya kwanza na mpenzi wake mpya

449
0
Share:
Share this
  • 853
    Shares

Baada ya wiki iliyopita kushare video akiwa na mpenzi mpya wakila bata mkoani Mtwara baada ya show ya Wasafi, Diamond Platnumz ameonekana hadharani akiwa na mpenzi wake huyo, Tanasha Donna Oketch.

Staa huyo wa Bongo ambaye alitumbuiza katika Uwanja wa Thika katika Wasafi Festiva alionekana hadharani kwa mara ya kwanza akiwa na mrembo huyo.

Tanasha alimpokea Diamond pamoja na wanamuziki wengine walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa ajili ya show ya Wasafi ambayo ilifanyika nchini Kenya siku ya Jumamosi.

Katika video zake alizoweka Instagram mapema wiki iliyopita, Diamond alimsifu Tanasha  akieleza kuwa amemfanya awe kwenye mapenzi zaidi ya mwanamke mwingine yoyote.

 

Comments

error: Content is protected !!