Picha: Mbunge Zitto amtembelea Samatta nyumbani kwake

364
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe Ruyangwa jana amemtembelea mchezaji wa soka la kulipwa anayeichezea timu ya KRC Genk ya nchini ubelgiji, Mbwana Ally Samatta.

Zitto alimtembelea Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), nyumbani kwake nchini Ubelgiji ambako ndiko anakoishi kwa sasa.

Kabla ya kumtembelea Samatta, Zitto alifanikiwa pia kumtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu anayeendelea na matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, nchini humo kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na risasi zaidi ya 36 na watu wasiojulikana, Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma.

Comments

error: Content is protected !!