Picha: Muonekano wa gari la Mwalimu Nyerere baada ya kukarabatiwa na VETA

470
0
Share:
Share this
  • 773
    Shares

Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kimekarabati gari alilokuwa akilitumiwa Mwalimu Nyerere katika harakati zake za kudai uhuru wa Tanganyika ikiwa ni njia ya kumuenzi Baba wa Taifa katika kumbukizi ya miaka 19 ya kifo chake.

Mwalimu Nyerere alifariki Oktoba 14 mwaka 1999 mjini London, Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu. Alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 29 Oktoba 1964 hadi 5 Novemba 1985 ambapo nafasi hiyo ilichukuliwa na Mzee Al Hassan Mwinyi.

Kila mwaka Oktoba 14 Tanzania ni siku ya mapumziko nchini Tanzania ambapo ni kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere.

Akizungumza katika Maonyesho ya Kitaifa ya Wiki ya Vijana yanayofanyika jijini Tanga, Mkurugenzi Mkuu wa VETA Nchini, Dk. Pancras Bujulu amesema kuwa, amefurahi sana kuona VETA imepewa nafasi ya kukarabati magari mawili aliyoyatumia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kwamba magari hayo yatakabidhiwa kwa serikali Oktoba 14.

“Gari hilo aina ya Austene yenye namba ya usajili MS 5480inahisiwa lilitengenezwa mwaka 1947, lilikuwa limehifadhiwa kwenye ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro.

“Kwetu ilikuwa kama fursa kwa vijana wetu kuonyesha namna walivyoiva kwenye ufundi  tukaliomba na kupatiwa na kwa sasa tumelitengeneza na linatembea,” amesema mkurugenzi huyo.

Dkt Bujulu amesema kuwa magari hayo yaliyokarabatiwa Mjini Moshi, yote yanafanyakazi vizuri, na yatajifadhiwa katika sehemu maalum za makumbusho ili kutunza kumbukumbu hiyo muhimu kwa taifa.

 

Comments

error: Content is protected !!