Polisi Dar watoa masharti kuhusu maeneo unayoweza kuvaa nguo fupi

701
0
Share:
Share this
CMTL Group

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na kueleza kuwa, mavazi hayo yanapaswa kuvaliwa katika maeneo maalum peke yake.

Marufuku hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanada Maalum wa Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa ambapo amesema moja ya maeneo ambayo mavazi hayo yanaweza kuvaliwa ni katika fukwe.

Mambosasa aliyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wakati akizungumzia mwenendo wa matukio ya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Amesema kwamba, Jeshi la Polisi linapofanya msako, huwatafuta wale wote ambao wanakiuka sheria, na kwamba kuhusu wanaovaa nguo fupi, kuna wale ambao wanajiuza lakini pia kuna wale wanaowahifadhi watu wanaojiuza ili kujipatia kipato. Mambosasa amesema kwamba, wote hao watachukuliwa hatua.

Aidha, akiendelea kutolea ufafanuzi suala hilo, alisema kwamba, polisi wakimkuta mtu amevaa nguo fupi kwenye fukwe hawatakuwa na shida naye kwa sababu ni mahala pake, lakini wakimkuta mtu huyo na mavazi hayo kanisani, msikitini au mahala pasipostahili, watamchukulia hatua.

Mambosasa alilazimika kuyasema hayo yote baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari kama jeshi hilo linaendesha msako dhidi ya watu wanaovaa nguo fupi.

Comments

error: Content is protected !!