Polisi wakiri kumuua kikongwe kwa risasi mkoani Mara

270
0
Share:
Share this
  • 337
    Shares

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki amethibitisha kuuawa kwa kupigwa risasi Mzee Edward Mahende (73) mkazi wa Kijiji cha Kenyana A wakati wakisaka mtuhumiwa wa wizi wa mifugo.

Mzee Edward ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wilayani Serengeti ambapo tukio hilo lilitokea Oktoba 12, 2018 saa 8 usiku nyumbani kwa marehemu.

Kamanda Ndaki amesema Mzee Edward alitoka na mkuki kwa lengo la kumchoma Inspekta wa Polisi aliyekuwa akipiga hodi katika nyumba hiyo.

Amesema marehemu alitoka akiwa na mkuki huo na askari walimshambulia kwa risasi na kufariki.

Comments

error: Content is protected !!