Producer wa Ali Kiba afichua siri kubwa ya wimbo wa Mvumo wa Radi

1667
0
Share:
Share this
  • 1.3K
    Shares
CMTL Group

Mtayarishaji maarufu wa muziki hapa nchini (Producer), Man Water kutoka Combination Sound ambae amekuwa akifanya kazi na wasanii tofauti tofauti hapa nchini akiwemo mkali wa Bongo Fleva ndani na nje ya Tanzania, Ali Kiba amefunguka siri nzito iliyojificha ndani ya wimbo wa Mvumo wa Radi.

Man Water ambaye ndiye ametengeneza wimbo wa Mvumo wa Radi wa Ali Kiba ambao uliachiwa hivi karibuni amesema kuwa anajiamini kwa alichokifanya ndani ya wimbo huo japokuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiusemea vibaya.

Man Water amesema akilinganisha nyimbo alizozitengeneza anaona kuwa amepanda kiwango kwani wimbo wa sasa ni mkali zaidi ya nyingine alizozitengeneza hapo awali.

Man Water amezungumzia vitu vilivyoufanya wimbi huo kuwa mkali ni pamoja na matumizi ya ‘live sounds’ pamoja na ubunifu na uthubutu uliopo katika wimbo huo.

“Naweza nikasema nimefanya muziki mzuri. Kama tunafanya ngazi ninkwamba nimepanda ngazi. Mvumo wa radi ni kali kuliko hata Seduce Me. Pale mi nazungumzia creativity iliyokaa pale, live sounds na nini. Kwaivyo mimi sibabaishwi na comment ya mtu ambaye hata ukimwambia ni nini kimefanyika pale hajui,” alisema Man Water alipokuwa akihojiwa na televisheni moja ya mtandaoni.

Producer huyo alieleza pia kitu ambacho alisema kuwa hajawahi kukieleza mahali popote pale kuwa, katika wimbo wa Mvumo wa Radi amewashirikisha waimbaji tofauti tofauti katika chorus pamoja na badhi ya vipande.

Man water amesema amefanya hivyo ikiwa ni ubunifu wake ili kuufanya wimbo huo uwe bora na hata Ali Kiba mwenyewe hakuwajua waimbaji hao.

“Katika Mvumo wa Radi kuna sauti ziimesikika. Sauti hizi hata Ali Kiba mwenyewe hawajui walioimba. Hiyo ni creativity ya producer. Pale kuna sauti yangu, kuna saut ya waimbaji kadhaa kutoka FM Academia. Lakini hata wale jamaa hawajawahi kupeana mkono na Alikiba. Wanamjua Alikiba lakini yeye mwenyewe hawajui mmoja mmoja. Lengo lilikuwa ni kutengeneza kitu kikubwa,” alisema.

Wimbo wa Mvumo wa Radi uliotoka hivi karibuni ulitarajiwa kufanya vizuri kuliko ilivyo sasa, lakini ulikumbwa na changamto kadhaa ikiwemo idadi ya watizamaji (viewers) katika mtandao wa youtube kutokuongezeka jambo ambalo lilitajwa kuwa  ni matatizo ya kiufundi.

Kama bado hujatazama video hiyo bofya hapa chini kuitazama.

Usisahau kushare na marafiki ili nao wapate kuburudika.

Comments

error: Content is protected !!