Rais Dkt Magufuli ampongeza Uhuru Kenyatta kwa ushindi

687
0
Share:
Share this
CMTL Group

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne Agosti 8 mwaka huu.

Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) alimtangaza Rais Uhuru Kenyatta mshindi jana Agosti 11 majira ya saa nne usiku baada ya matokeo hayo ya uchaguzi uliogubikwa na ushindani mkubwa kusubiriwa kwa hamu na watu mbalimbali.

Katika salamu za pongezi alizotoa Rais Dkt Magufuli, amemtakia mafanikio mema Rais Kenyatta katika kipindi kingine cha uongozi wake.


Mbali na Rais Magufuli, viongozi wengine waliompongeza Rais Kenyatta kwa ushindi huo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Nkurunziza wa Burundi, Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Comments

error: Content is protected !!