Rais Magufuli afunga mjadala wa elimu ya RC Makonda

1617
0
Share:
Share this
  • 1.7K
    Shares

Rais Dkt Magufuli leo amefunga rasmi mjadala kuhusu vyeti na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kusema kuwa anaridhishwa na utendaji wake na kwamba kwake anamuona ni msomi mzuri.

Kauli hiyo ya Rais Dkt Magufuli imekuja baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari zikidai kuwa, Paul Makonda alifeli kidato cha nne na hivyo aametumia vyeti vya mtu mwingine. Wanaotoa hoja hizo, wamekuwa wakishinikiza Rais Magufuli kumfuta kazi kiongozi huyo wa mkoa kwa kosa la kughushi vyeti.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT), Rais Magufuli amewakosoa wanaomnyooshea kidole Makonda na kusema kwake yeye ni msomi.

“Wanasema hajasoma, mimi hata kama hajui A ila anakamata madawa ya kulevya, kwangu ni msomi mzuri,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amempongeza RC makonda kwa namna anavyofanya kazi na kutatua changamoto za wananchi, hatua iliyomfanya kuwasihi wakuu wengine wa mikoa kuja kujifunza kwake.

“”Namuona RC Makonda anavyohangaika,Waziri mkuu waambie wakuu wa mikoa mingine waje wajifunze kwake.”

Comments

error: Content is protected !!