Rais Magufuli ateua Mwenyekiti na Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma

285
0
Share:
Share this
  • 338
    Shares

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Steven Bwana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka 3.

Pamoja na kumteua mwenyekiti wa tume, Mhe. Rais Magufuli amewateua Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Walioteuliwa ni;

  1. George D. Yambesi
  2. Balozi Mstaafu John Michael Haule
  3. Immaculate P. Ngwale
  4. Yahaya F. Mbila
  5. Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay.

Uteuzi huu wa Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma umeanza tarehe 22 Novemba, 2018.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

04 Desemba, 2018

Comments

error: Content is protected !!