Rais wa 41 wa Marekani afariki dunia

309
0
Share:
Share this
  • 370
    Shares

George Herbert Walker Bush, Rais wa 41 wa Marekani na baba mzazi wa George W. Bush, Rais wa 43 wa Marekani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 baada ya afya yake kutokuwa imara kwa muda sasa.

George H.W. Bush ambali amefariki jana Novemba 30, 2018 mbali na kuwa Rais wa Marekani mwaka 1989 hadi 1993, amewahi kuwa Makamu wa Rais kwa muda wa miaka 8, amekuwa Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) mwaka 1976 pamoja na rubani wa ndege za jeshi la nchi hiyo.

Rais huyo atakumbukwa kwa kuiongoza Marekani kuelekea mwishoni mwa Vita vya Baridi (Cold War) kulikopelekea kuanguka kwa Urusi na ukuta wa Berlin na kuiona Marekani ikijikita kileleni kama kiongozi wa dunia.

Alizaliwa Milton, Mass Juni 12, 1924 akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto watano wa Prescott Bush na Dorothy Walker.

Comments

error: Content is protected !!