Serikali yaagiza kuchunguzwa kwa taasisi inayotoa mikopo kwa wanafunzi

623
0
Share:
Share this

Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeviagiza vyombo vya dola kuichunguza Taasisi ya Msaada wa Kijamii Tanzania (TSSF) kwa tuhuma za utapeli.

Viongozi wa taasisi hiyo wanashikiliwa na Jeshi la polisi ikiwa ni muda mchache tokea walipomaliza mahojiano na Wizara ya Elimu.

Taasisi hiyo inatuhumiwa kuwatoza wanafunzi fedha kiasi cha sh. 30,000 kama gharama za maombi ya mkopo wakati wizara haiitambui na haijapewa usajili rasmi wa kufanya jambo hilo.

Aidha Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako alisema bungeni Novemba 10, mwaka huu kuwa Wizara ya Elimu haiitambui taasisi hiyo na aliwatahadharisha watanzania kuwa makini na taasisi hiyo na watalifanyia kazi kujua uhalali wake wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

“Nieleze kwa masikitiko kwamba nimepewa gazeti, sasa hivi ambalo linaonyesha tangazo kwamba hii taasisi inawatangazia wanafunzi na inawachaji sh. 30,000 na wanasema kutakuwa na mkutano ambao mgeni rasmi atakuwa waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako. Siitambui hii taasisi, hawajanikaribisha na wala tarehe ya mkutano,” alisema Waziri Prof. Ndalichako.

Comments

error: Content is protected !!