Sheikh Ponda atakiwa kujisalimisha mwenyewe Polisi

489
0
Share:
Share this
CMTL Group

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amemtaka Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda kujisalimisha ndani ya siku tatu kuanzia leo Alhamisi Oktoba 12 kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi.

Kamanda Mambosasa amemtaka kiongozi huyo kujisalimisha mwenyewe katika Kituo cha Kikuu cha Polisi kwani baada ya muda uliotolewa, watamtafuta popote alipo.

Mambosasa ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kiongozi huyo alitenda kosa hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika mkutano huo, Sheikh Ponda alitoa lugha ya uchochezi na kejeli dhidi ya serikali akijua kabisa kwamba anachokifanya ni kosa.

Jana Polisi walifika katika eneo alipofanyia mkutano na kuwachukua baadhi ya waandishi wa habari na wafausi wake, tukafanya nao mahojiano, kisha tukawaachia huru, alisema Mambosasa.

Amemsisi Sheikh Ponda kutokukimbia na kwamba ni heri afike kwa ajili ya mahojiano.

Comments

error: Content is protected !!