Shilole ameamua kusoma Kiingereza na wataalamu wa lugha duniani

842
0
Share:
Share this

Baada ya kuchekwa sana kwa kutojua Kiingereza, msanii wa bongo flava Shilole ameingia mkataba na Shirika la Uingereza (British Council Tanzania) ili kujifunza lugha hiyo. Mbali ya muziki, msaani huyo anajulikana sana kwa kuwa na hamasa ya kuongea Kiingereza bila kujali makosa ambayo anayafanya. Wiki iliyopita tuliona video iki-trend ya mwanadada huyo akijaribu kusema “Subscribe” alivyokua anaongelea kuhusu mwimbo wake mpya.

Shirika la Uingereza (British Council Tanzania), limefurahi Shilole ameamua kutaka kujiendeleza katika lugha hiyo ambayo itamsaidia katika kazi yake kama msanii hususani kumpa fursa za kimataifa zaidi.

Angela Hennelly ambaye ni kiongozi wa shirika hilo hapa nchini (Country Director), amesema kuwa ni fursa nzuri kwa Shilole kujua lugha ya Kiingereza na amempongeza kwa hatua hiyo aliyoichukua. Ameendelea kusema kuwa hii itamfungulia milango mingi ya fursa kulingana na jinsi uchumi wa dunia unavyokua na changamoto wanazozipata haswa wasanii.

Angela ameendelea kusema kuwa anategemea hii fursa itawapa moyo vijana kufikiria pia kujiendeleza katika lugha ili waweze kufanya mawasiliano kwa urahisi katika shughuli zao za kila siku haswa kwa upande wa ajira.


Comments

error: Content is protected !!