Simulizi ya shuhuda namna kifo cha Pancho Latino kilivyotokea baharini

701
0
Share:
Share this
  • 740
    Shares

Mmoja wa mashuhuda ambaye pia ni dereva wa mtumbwi ameelezea namna kifo cha mtayarishaji wa Muziki Pancho Latino kilivyotokea kwa kusema kuwa, alimuona akiwa ndani ya maji, na alipowaambia rafiki zake (Pancho Latino) waliokuwa wamefuatana naye, walimwambia anajua kuogelea hivyo amwache kwani huo ndio uogeleaji wake.

Shuhuda huyo baada ya muda wa dakika 10 alilazimika kwenda alipokuwa Pancho kwani alimuona amekaa ndani ya maji kwa muda wote huo bila hata kuinua kichwa, jambo ambalo ni gumu kufanya kama mtu anaogelea kawaida.

Amesema kuwa walizama ndani ya maji na kukuta maji yakiuchukua mwili wa Pancho kuupeleka palipo na kina kirefu (deep sea) kwani tayari alikuwa ameshafariki dunia.

Aidha, akizungumza kinachoweza kuwa chanzo cha kifo cha mtayarishaji huyo wa muziki nchini Tanzania, shuhuda huyo alisema huenda pombe ikawa ni sababu kubwa, kwani baada ya kuuopoa mwili huo kutoka baharini na kuugandamiza, pombe nyingi ilitoka. Hivyo huenda alizidiwa na pombe wakati akiogelea.

Baada ya kuutoa mwili huo baharini walitumia boti ya serikali kumwahisha hospitalini Kunduchi, ambapo alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Lugalo.

Pancho Latino atakumbukwa kwa kazi zake nzuri katika muziki wa Tanzania, ambapo miongoni mwa ngoma kali alizowahi kutengeneza enzi za uhai wake akiwa katika Studio za B’Hits ni pamoja na Usije Mjini: AY na Mwana FA Here We Go: Wakacha Higher: Nikki II Dar es Salaam Stand Up: Chid Benz Bye Bye: Joh Makini Press Play: DJ Choka, Karibu Tena: Joh Makini.

Sikiliza hapa moja ya kazi za Pancho Latino. Ni wimbo wa Joh Makini aliomshirikisha G Nako- Bye Bye

 

Comments

error: Content is protected !!