Sweden yamuita Balozi wa Tanzania, Dkt Slaa kwa mahojiano

605
0
Share:
Share this
  • 522
    Shares

Balozi wa Tanzania nchini Sweden aliitwa na Wizara ya Mambo ya Nje nchini humo kwa ajili ya mahojiano kufuatia kuminywa kwa demokrasia nchini Tanzania pamoja na kampeni dhidi ya ushoga iliyoanzishwa hivi karibuni na kupelekea nchi kukosolewa na jumuiya za kimataifa.

Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Patric Nilson amesema kuwa Dkt Wilbrod Slaa aliitwa na kuelezwa kuwa, Sweden inasikitishwa na hatua zisizo za kidemokrasia zinazochukuliwa na mamlaka nchini Tanzania, na kupelekea kuathiri utawala wa sheria na haki za binadamu. Pamoja na hayo, Balozi Dkt Slaa alielezwa pia kuhusu kampeni dhidi ya ushoga.

Mbali na Sweden, nchini nyingine wananchama wa Umoja wa Ulaya (EU) zimechukua hatua za kufanana na hizo, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukwaji wa misingi ya demokrasia.

Novemba 7 mwaka huu, Balozi wa EU, Roeland van de Geer aliondoka nchini kwa kile umoja huo ulichoeleza kuwa alifukuzwa, baada ya kupingana na namna hatua dhidi ya ushoga zilivyokuwa zikichukuliwa.

Baadhi ya taasisi na nchi nyingine ikiwemo Denmark, zimezuia fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Tanzania, kwa kile walichoeleza kuwa ni kuminywa kwa demokrasia, hasa kubwanwa kwa mazingira ya asasi za kiraia, vyombo vya habari na vyama vya siasa.

Comments

error: Content is protected !!