Taarifa ya Polisi kuhusu waliomteka mfanyabiashara MO Dewji

571
0
Share:
Share this
  • 1.2K
    Shares

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa taarifa ya awali kuhusu tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji (Mo) ambapo ameeleza kuwa, waliohusika katika tukio hilo la utekaji ni watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

Mo ametekwa na watu hao mapema leo asubuhi wakati akienda kufanya mazoezi Collesium Gym iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema kwamba wameweka vizuizi kuhakikisha hakuna mtu anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi.

Dereva wa Uber (jina linahifadhiwa) amesema aliona  watu wakishuka kwenye gari dogo, Hoteli ya Collessium wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mfanyabiashara huyo.

Comments

error: Content is protected !!