Tabia 5 ambazo hupaswi kuzivumilia katika uhusiano wa kimapenzi

721
0
Share:
Share this
  • 987
    Shares

Wahenga wanaomsemo unaosema kuwa, aliyependa hashauriki. Msemo huu unaukweli ndani yake kwa sababu kuna watu wanafanya mambo hadi unajiuliza, alikuwa ana waza nini? Ukweli ni kwamba uhusiano unaweza ukawa ni jambo la kukufanya uwe na furaha na ukaliwaza kila siku, lakini hali inaweza kubadilika hadi ukatamani muachane kutokana na maumivu unayopitia. Makala hii italezea tabia tano ambazo hupaswi kuzivumilia katika uhusiano.

5. Kutawaliwa

Related image

Sina hakika kama hilo ndio jina bora la kuipata tabia hii, lakini suala kubwa hapa ni kwamba mnapokuwa katika uhusiano, mnakuwa mpo watu wawili. Sasa asiwepo mtu yeyote ambaye maamuzi yote anafanya yeye mwenyewe kwamba akishaamua, basi mwingine hana cha kufanya zaidi ya kufuata tu. Kama hali iko hivi hakikisha unabadilika, wewe sio mwenye hatimiliki ya uhusiano wenu, nyote mna nguvu sawa na linapokuja jambo mjadiliane hadi mfikie muafa. Ukiona mnazungumzia nyumbani mwenzako haelewi, nenda naye mahali, nunua kahawa, kunyweni huku mnazungumza.

4. Mawazo hasi

Image result for negative vibes couple

Mawazo hasi huharibu kila kitu kuanzia masuala yako ya kazi hadi maisha binafsi. Mpenzi wako anapaswa kuwa mtu wa kukupooza na kukushauri pale unapokumbana na changamoto katika kazi au eneo jingine, lakini asiwe mtu wa kuongeza mzigo juu ya mzigo, mtu asiyejali chochote. Kama hali iko hivi, hakikisha unatafuta suluhisho na kwamba furaha yako isihusianishwe na mtu mwingine bali itokane na wewe mwenyewe.

3. Ugomvi

Ugomvi katika uhusiano unaweza kuwa wa kimwili au kiakili. Tatizo kubwa ni kwamba, ugomvi unapotokea watu huwa hawachukua hatua stahiki na kusema kwamba yatapita tu. Hilo si suluhisho la tatizo unahitaji msaada. Ugomvi wa aina yoyote katika uhusiano haukubaliki. Kama mwenza wako huwa anakupiga, tafuta ushauri wa wazazi au wakisheria kuweza kuondokana na tatizo hilo. Kama ugomvi ni wa kisaikolojia, hakikisha unafikia uamuzi kwamba uhusiano wenu utaendelea endapo tu atabadilika.

2. Ujinga

Inahitaji nguvu kubwa sana kujenga uhusiano wenye tija. Hii hujumuisha kusaidiana na kujengana kimawazo kwa  kushauriana na kuwa pamoja katika hali zote za huzuni na raha. Kila mtu huhitaji mtu wa karibu wa kimsikiliza hasa pale anapokuwa na jambo linauchoma moyo wake. Lakini ukiona mwenzako hawi karibu na wewe au hakujali na kuanza kutoa sababu ndogo ndogo kama vile, nilikuwa busy na kazi, sikukumbuka, sikuwa na muda, hakika huy0 ni mjinga na ujinga huo usivumiliwe. Hii inaonesha kwamba kuna tatizo kwenye uhusiano wenu na kwamba lazima litatuliwe. Kama haoneshi ushirikiano, na wewe anza kufanya mambo yako. Kumbuka, hakuna mtu aliyeweza kuwa busy kiasi kwamba asipate muda wa kumjali ampendae.

1. Kukatisha tamaa

Image result for black guy shouting to a woman

Kutofautiana ni jambo la kawaida katika uhusiano, hakuna mtu anategemea kila siku mtakuwa mko vizuri. Kuna hatua inafika mtu anasema vitu ambavyo pengine hakupaswa kuvisema na anatakiwa kuomba msamaha baada ya hapo. Lakini kama mwenzako anatoa maneno ya kukukwaza kila mara hata kama hamna ugomvi au anakukatisha tamaa kwenye kila unachojaribu kufanya badala ya kukutia moyo na kukusaidia ufanikiwe, hapo kuna tatizo. Hakuna anayependa kunenewa maneno hasi, hivyo kama hiyo ni tabia ya mwenzako, hakikisha anabadilika.

Je! Ni tabia gani nyingine ambazo wewe unadhani watu hawapswi kuzivumilia? Andika hapo chini kwenye kisanduku cha maoni ili kuweza kuelimisha wengine.

 

Comments

error: Content is protected !!