Tangazo la nafasi za kazi kutoka Uhuru Publications Limited

633
0
Share:
Share this
CMTL Group

Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), wachapishaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:

  1. KAZI: Afisa Matangazo (Freelancer)

2. VITUO VYA KAZI: Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Lindi na Mtwara.

3: MAJUKUMU: Kutafuta matangazo kutoka Ofisi za Serikali, mashirika ya Umma, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), kampuni binafsi, n.k. kwa ajili ya kuyachapisha kwenye magazeti yetu.

4. SIFA ZA MWOMBAJI: Awe na Elimu ya Kidato cha Nne, au zaidi. Awe na uzoefu wa kutafuta matangazo usiopungua miaka miwili.

5. MSHAHARA: Malipo ya kazi hii yatalipwa katika mfumo wa kamisheni kulingana na thamani ya tangazo.

6. JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Barua za maombi zikiambatana na habari binafsi (CV), vyeti vya shule, n.k zitumwe kwa anwani ifuatayo:

Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala,

Uhuru Publications Limited,

S.L.P 9221

Email: uhurunews@yahoo.com

Fax No. 2183780

DAR ES SALAAM

Mwisho wa kupokea maombi: Tarehe 28/02/2018

Chanzo: Gazeti la Uhuru toleo la Jumatatu, Februari 12, 2018, ukurasa wa 28.

Comments

error: Content is protected !!