TANZIA: Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru afariki dunia Muhimbili

1274
0
Share:
Share this
  • 827
    Shares

Dar es Salaam: Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wa marehemu, Kinje Ngombale amethibitisha kutokea kifo hicho.

Mwanasiasa huyo mkongwe alifikishwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es Salaam na alifanyiwa upasuaji Januari 4.

Mapema Januari mwaka huu, Mke wa Mzee Kingunge, Peres Kingunge alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kupooza.

Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wachache waliosalia ambao walishiriki katika kupigania uhuru wa Tanzania pamoja na Mwalimu Nyerere.

Mzee Kingunge alizaliwa Mei 30, 1930 na hadi mauti inamkuta alikuwa mwananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

 

Comments

error: Content is protected !!