Teknolojia: Mtandao wa WhatsApp wafanya marekebisho mengine

1442
0
Share:
Share this
  • 1.2K
    Shares
CMTL Group

WhatsApp imekuwa mstari wa mbele kuleta vitu vya kuvutia kwenye programu tumishi maarufu zaidi duniani kwa kurahisisha mawasiliano na sasa wameleta kitu kizuri kwa wale ambao wanachukizwa na kubadilishwa badilishwa kwa taarifa za kundi.

Kwenye WhatsApp katika kipengele cha kundi ni jambo la kawaida sana kwa mtu yeyote yule kuweza kubadilisha jina la kundi/kichwa cha habari au picha kwenye kundi husika. Lakini kitendo hicho sasa kimekomeshwa kwani katika sasisho la sasa la WhatsApp; kiongozi wa kundi ana uwezo wa kuruhusu mtu yeyote yule kubadilsha jina la kundi/picha au kuruhusu baadhi ya watu tu ndio waweze kurekebisha taarifa mbalimbali za kwenye kundi husika.

Sasa wewe kama kiongozi wa kundi kwenye WhatsApp inabdi uingie Group info > Group settings > Edit group info ili kuweza kuamua kile ambacho utapenda kundi unaloliongoza lisiwe na uwezo wa kubadilisha taarifa (picha/maelezo) kadri wapendavyo.

Maboresho haya yamefanywa kwa watumiaji wote wa mtandao wa WhatsApp wanaotumia vifaa vya Androis, IOS pamoja na Windows.

Masasisho mengine yanatarahiwa kuletwa kwenye programu tumishi yenye watumiaji zaidi ya watu bilioni moja. Moja ya vitu hivyo ni kiongozi wa kundi kuzuia kila mtu kwenye kundi kuweza kutuma chochote au kuteua baadhi tu ya watu kuweza kuwasiliana kwenye kundi husika.

Comments

error: Content is protected !!