Ufafanuzi wa CHADEMA kuhusu ‘mgogoro’ kati ya Mbowe na Katibu Mkuu Dkt Mashinji

359
0
Share:
Share this
  • 495
    Shares

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt Vincent Mashinji, wametofautiana kwenye kikao cha kamati kuu.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa viongozi hao wa ngazi ya juu ya chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania, walitofautiana kwenye kikao cha kamati kuu kilichofanyika nyumbani kwa mwenyekiti (Mbowe) mwishoni mwa juma.

Kupitia wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema, chama hicho kimesema hakuna kikao chochote cha kamati kuu ambacho kimefanyika mwishoni mwa wiki, sio tu nyumbani kwa Mwenyekiti Mbowe bali popote pale.

Pia kulingana na utaratibu wa chama hicho, haijawahi kutokea wakati wowote vikao vya kamati kuu vikafanyika nyumbani kwa menyekiti wa Taifa.

Aidha, ameongeza kwamba, hakuna popote ambako viongozi hao waandamizi wametofautiana kuhusu yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii, huku akiwaomba watanzania na wanachama wa chama hicho wapuuze taarifa hiyo potofu inayosambazwa kwenye mitandao.

 

 

 

Comments

error: Content is protected !!