Ufafanuzi wa Vodacom ndugu yako akifariki na kuacha fedha M-Pesa

1605
0
Share:
Share this
  • 1.1K
    Shares
CMTL Group

Kampuni ya maswasiliano ya Vodacom nchini Tanzania imetoa maelekezo kwa ndugu wa marehemu kuweza kupata fedha zilizopo kwenye akaunti ya M-Pesa baada ya mwanafamilia aliyekuwa anatumia mtandao huo kufariki dunia.

Vodacom wamelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter kuuliza, nini kitatokea kwenye fedha zake zilizopo M-Pesa endapo atafariki dunia.

Katika majibu hayo, Vodacom wameeleza kuwa, endapo mwanafamilia akifariki dunia na kuacha fedha zake, ndugu mmoja atatakiwa kutembelea duka la vodacom lililopo karibu akiwa na nyaraka muhimu.

Mtu huyo ni lazima awe ndege wa karibu kabisa na marehemu, na baada ya kukamilisha taratibu zote za msingi zinazotakiwa, atapatiwa fedha hizo.

“Habari, kuna akaunti ambayo inahifadhi pesa hizo, hivyo kama hautakuwepo leo hii,basi ndugu zako watatembelea duka letu la vodacom na kitambulisho chake, cha kwako na cheti cha kifo chako na atapatiwa msaada. Ila nanatakiwa awe ndugu yako wa karibu kabisa^GL,” waliandika Vodacom.

Licha ya ufafanuzi huo, baada ya watumiaji wa mtandao huo walilalamika kuwa, wakiacha kutumia kadi zao za simu kwa kipindi cha miezi mitatu, wanakuta namba zao zinatumiwa na watu wengine na hivyo kupoteza fedha zilizokuwa katika akaunti zao za M-Pesa.

Comments

error: Content is protected !!