UGANDA: Mrembo anaswa kwenye kaburi la Mowzey Radio

549
0
Share:
Share this
CMTL Group

Polisi nchini Uganda wananshikilia msichana anayeitwa Maureen Namuli, baada ya kukutwa akicheza juu ya kaburi la aliyekuwa mkali wa muziki nchini humo, Mowzey Radio.

Radio alizikwa kijijini kwao Kagga, Nkawauka wiki iliyopita ndipo juzi mrembo huyo alipoonekana akicheza cheza kwenye kaburi hilo, jambo ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

Baada ya kutiwa mbaroni, Maureen alipandishwa kwenye gari la polisi huku akiimba nyimbo za Radio, kisha akapelekwa katika Hospitali ya Butabika ili kupimwa afya ya akili.

Msanii Mowsey alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuangushwa chini na baunsa wa klabu ya De Bar kutokana na kuwepo kwa majibizano na ugomvi baina yao.

Hata hiyo baunsa huyo anayejulikana kwa jina, George Wamala tayari amekamatwa na jeshi la polisi nchini humo na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Mowzey.

Comments

error: Content is protected !!