Uwekezaji wazidi kushamiri Tanzania

1137
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe amesema uwekezaji unazidi kushamiri nchini Tanzania na TIC inahakikisha wawekezaji wanaendesha shughuli zao vizuri na kwa faida.

Bw. Mwambe amesema hivi TIC imeondoa dosari zote zilizokuwa zinawakwaza wawekezaji na kwamba mwekezaji mpya anakamilisha mchakato wote wa kupata vibali na nyaraka nyingine za kumwezesha kuwekeza ndani siku tatu na kila huduma inapatikana ndani ya Ofisi ya TIC (One Stop Center). 

Bw. Mwambe ameongeza kuwa kauli za kuwa hali ya uwekezaji Tanzania ni mbaya ni za uzushi na zenye nia ya kuchafua sifa ya Tanzania ambayo kwa ni moja ya nchi 10 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi duniani kwa wastani wa asilimia 7.2, na ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji Afrika Mashariki.

Amesema ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania imepata uwekezaji wa Dola za Marekani Bilioni 1.35 sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 3 za Kitanzania, ikifuatiwa na Uganda iliyopata uwekezaji wa Dola za Marekani Milioni 537 ambao ni chini ya nusu ya Tanzania.

Bw. Mwambe ameongeza kuwa pamoja kuwepo kwa hali nzuri ya uwekezaji TIC inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwavutia wawekezaji na kuwaeleza fursa mbalimbali muhimu ikiwemo uwepo wa soko la uhakika la ndani ya nchi na nje ya nchi, vivutio vya uwekezaji vinavyotolewa na TIC pamoja na ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza.

Comments

error: Content is protected !!