Video: Diamond azungumzia sakata la Hamisa Mobeto kwenda kwa mganga kumloga

933
0
Share:
Share this
  • 243
    Shares

Tangu jana kupitia mitandao ya kijamii pamoja na WhatsApp kumekuwa na sauti zikisambazwa ambazo zinasemakana ni za Hamisa Mobeto akiwa kwa mganga katika kile kinachodaiwa kuwa ni kwa ajili ya kumloga Diamond ili ampende zaidi na aolewe naye.

Kumekuwapo na mkanganyiko kuhusu sauti hizo huku baadhi ya watu wakisema kuwa si Hamisa, bali ni watu wameiga sauti yake kwa lengo la kumchafua, wakati wengine wakisema ni Hamisa.

Kufuatia mkanganyiko huo, mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye ni mhusika mkuu katika hili amezungumza na kusema kwamba anafahamu kuhusu suala hilo na alishamuonya mhusika.

Licha ya kuwa watu wamekuwa wakimtaja Hamisa Mobeto, lakini Diamond yeye hakutaja jina lakini akasema kuwa mhusika anajifahamu na kwamba ameshamuonya baada ya kujua kuwa amekuwa akiwatumia watu waseme kwamba sauti hiyo imetengenezwa na mama yake pamoja na dada yake, Esma Platnumz.

Msikilize Diamond hapa chini akielezea kisa kizima;

Comments

error: Content is protected !!