VIDEO: Mbunge Mstaafu wa Kilombero amshukuru Rais Magufuli kwa msaada aliompa

428
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mbunge mstaafu wa Kilombero, Abdul Rajabu Mteketa amepelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu, baada ya Jumamosi Februari 11, 2018 kuomba msaada wa kupatiwa matibabu ya upasuaji wa magoti yake.

Mbunge huyo aliyetumikia jimbo la Kilombero baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka 2010, alitumia njia ya video mtandaoni kupeleka ujumbe kwa Rais na jana Jumapili gari la wagonjwa lilifika na kumchukua kumpeleka Muhimbili.

Mbunge huyo amemshukuru Rais Magufuli kwa msaada mkubwa aliompatia kwani kutokana na hali aliyo nayo wao wenyewe wasingeweza kujigharamia.

Hapa chini ni video ya Mbunge Mstaafu, Abdul Rajabu Mteketa akimshukuru Rais Magufuli.

Comments

error: Content is protected !!