Video: Vijue viwanda vitano vikubwa Rais Magufuli atakavyovizindua kesho Pwani

8829
0
Share:
Share this
CMTL Group

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 20 Juni, 2017 anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Pwani.

Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atazindua viwanda vikubwa vitano ambavyo ni kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd), kiwanda cha matrekta (Ursus-TAMCO Co. Ltd), kiwanda cha chuma (Kiluwa Steel Group), kiwanda cha kukausha matunda (Elven Agric Company) na atafungua kiwanda cha vinywaji baridi (Sayona Fruits).

Pia Mhe. Rais Magufuli atazindua mradi wa maji wa Ruvu na barabara ya Bagamoyo – Msata.

Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atakutana na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Juni, 2017

Comments

error: Content is protected !!